FOMU ya Maombi ya NIDA Download



FOMU ya Maombi ya NIDA Download

FOMU ya Maombi ya NIDA kwa Raia wa Tanzania, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ina jukumu muhimu nchini Tanzania, kwani inasimamia usajili na utoaji wa Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa raia wote wenye umri wa miaka 18 na zaidi.

Fomu ya NIDA 1A ni fomu ya maombi ambayo mtu yeyote anayetaka kupata kitambulisho anatakiwa kuijaza.

Fomu hii ni hatua ya kwanza na muhimu katika mchakato mzima wa kupata kitambulisho cha Taifa.

Kupitia kitambulisho cha taifa (Kitambulisho cha NIDA), raia wa Tanzania wanaweza kupata huduma mbalimbali za serikali na zakijamii kwa urahisi zaidi, kama vile kusajili laini za simu, kufungua akaunti za benki, kupata hati za kusafiria, na hata kununua ardhi.

 

Aidha, kitambulisho cha taifa cha NIDA ni nyenzo muhimu katika kuimarisha usalama wa raia na taifa kwa ujumla, kwani inasaidia katika kutambua uhalali wa mtu na kuzuia vitendo vya uhalifu mtandaoni na mtaani.

Kupitia Makala hii utafahamu jinsi ya kujaza Fomu hii na hatua zingine zote muhimu katika mchakato wa maombi ya NIDA ili kurahisisha mchakato huu kwa kila Mtanzania anayehitaji kitambulisho cha Taifa (NIDA)

BONYEZA HAPAKUDOWNLOAD FOMU YA MAOMBI YA NIDA

ILI KUJAZA FOMU HII NI LAZIMA IJAZWE NA RAIA WA TANZANIA KWA WINO MWEUSI.

Hizi hapa ni taarifa zinazohitajika Wakati Kujaza Fomu hii.

Hakikisha una taarifa hizi zote kabla ya kuanza kujaza fomu ili kurahisisha mchakato na kuepuka makosa.

Taarifa zako Binafsi zinazohitajika.

·         Jina lakoa kwanza, la kati, na la Ukoo

·         Majina yako mengine (kama yapo)

·         Tarehe yako ya kuzaliwa

·         Namba ya cheti cha kuzaliwa

·         Mahali ulipozaliwa

·         Jinsia

·         Hali ya Ndoa

·         Taarifa za Elimu (shule ya msingi, wilaya, mwaka wa kuhitimu)

·         Kazi na jina la mwajiri (kama umeajiriwa) Pamoja na

·         Namba yako ya Simu.

Taarifa za Wazazi Wako zinazohitajika

·         Majina ya kwanza, ya kati, na ya Ukoo ya Baba yako na Mama yako.

·         Tarehe za kuzaliwa za Baba na Mama

·         Nchi walikozaliwa Baba na Mama

Taarifa za Uraia Wako zinazohitajika

·         Uraia (kuzaliwa, Kurithi, au Kujiandikisha)

·         Namba ya cheti cha kujiiandikisha (kama ipo)

Mahali Unapoishi panahitajika

·         Namba ya nyumba, jina la Mtaa/Kijiji/Shehia, Kitongoji au Barabara

·         Mkoa, Wilaya, Kata/Nchi

·         Sanduku lako la Posta kama lipo

Anuani yako ya Makazi ya Kudumu inahitajika

·         Mkoa, Wilaya, Kata/Kijiji/Mtaa/Shehia, Kitongoji au Barabara

·         Nchi, Sanduku la Posta kama lipo.

Kumbukumbu zako Binafsi zinahitajika

·         Namba ya kitambulisho cha Taifa cha Baba na Mama

·         Namba ya Pasipoti

·         Namba ya Leseni ya Udereva

·         Namba ya kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi

·         Namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN) TRA/ZRB

·         Namba ya Uanachama wa bima ya afya

·         Aina ya mfuko wa hifadhi ya Jamii na namba ya uanachama

·         Namba ya cheti cha elimu ya sekondari na sekondari ya juu

·         Namba ya kujiandikisha kupiga kura (NEC/ZEC)

Hivi hapa ni vitu vinavyohitajika Wakati wa Kutuma Maombi ya Kitambulisho NIDA

1.    Cheti cha kuzaliwa

2.    Cheti za elimu ya msingi,

3.    Pasi ya kusafiria (Pasipoti)

4.    Cheti cha Elimu ya sekondari (kidato cha iv na vi)

5.    leseni ya Udereva

6.    Kadi ya Bima ya afya

7.    Kadi ya mfuko wa hifadhi ya jamii

8.    Kadi ya mpiga Kura

9.    Nambari ya mlipa kodi (Tin Number)

10. Kitambulisho cha mzanzibar mkazi

11. Barua kutoka kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa

Previous Post
No Comment
Add Comment
comment url